Pigo kwa PSG baada ya Cavani, Mbappe kujeruhiwa

Pigo. Klabu ya Paris St-Germain imekumbwa na pigo baada ya wachezaji wawili Kylian Mbappe na Edinson Cavani kupata majeraha katika ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Toulouse, Ligue 1.
Cavani aliondoshwa uwanjani dakika 14 za mwanzo wakati Mbappe alitolewa uwanjani kipindi cha pili.
Waswahili husema unapopata matatizo mwezako hutumia matatizo hayo kukuadhibu ama ni fursa kwake ndivyo ilivyo kwa Eric Maxim Choupo-Moting ambaye alichukua nafasi ya Cavani baada ya kuumia akafunga goli mbili kwenye mchezo huo.
Kasi ya PSG ya kushambulia ilipelekea, Mathieu
Goncalves akajifunga kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara akisaidia goli la tatu.
Angel di Maria alikosa penati kwenye mchezo huo licha ya makosa yake kusawazishwa na goli la mwisho la mlinzi wa Kibrazil Marquinhos.
Kocha Thomas Tuchel bado ameendelea kumkosa mchezaji wao ghali Neymar Jr ambaye bado hatima yake haijafahamika kama atasalia PSG au ataenda kwingineko, kuumia kwa wawili hao kunazidi kutoa mashaka kwenye kikosi cha matajiri wa Ufaransa.
Matokeo hayo yanaisogeza PSG mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligue 1 nyuma na Lyon na Rennes.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends