Pogba alengwa katika ujumbe wa kibaguzi baada ya kukosa penati

54
Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Paul Pogba amekuwa mchezaji wa tatu kukumbwa na ubaguzi wa rangi ndani ya wiki moja kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukosa penati kwenye mchezo wao dhidi ya Wolverhampton Wanderers Jumatatu.
Pogba, 26, alikosa penati katika kipindi cha pili na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Siku ya Jumapili mshambuliaji wa Reading Yakou Meite, 23,  alikumbwa na kadhia hiyo baada ya kukosa penati katika dakika za lala salama za mchezo dhidi ya Cardiff ilikuwa dakika ya 91.
Katikati ya wiki iliyopita mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham alijikuta katikati ya hisia za ubaguzi pia wa rangi baada ya kukosa penati ya mwisho kwenye mchezo wa Super Cup dhidi Liverpool.
Baada ya mtanange huo, ujumbe uliokuwa unamwelezea Pogba ulisambaa kupitia mtandao wa Twitter licha ya kuanza kufutwaa baada ya Kampuni hiyo kugundua zinamkebehi Mfaransa huyo na Kampuni husika ya Twitter kwa kuwa kinyume na utaribu wao.
Kanuni za Twitter zinasema “Watachukua hatua kali dhidi ya matumizi mbaya ya lugha kwenye mtandao wao”.
Mwezi Julai, Taasisi inayojihusisha na upingaji wa ubaguzi wa rangi Kick It Out walizalisha ripoti inayoonyesha kuongezeka kwa matukio ya ubaguzi kwa asilimia 43 ambapo kesi 274 zilipatikana msimu uliopita, zaidi ya 192 zilitokea misimu ya nyuma.

Author: Bruce Amani