Porto yajiweka kifua mbele dhidi ya Juventus, yaifunga 2-1

Porto ilifunga bao katika dakika ya kwanza ya kila kipindi cha mchezo wao wa jana na kujiweka kifua mbele katika mechi yao ya Champions League dhidi ya Juventus.

Mehdi Taremi aliichukua pasi mbovu ya Rodrigo Bentancur ya kumrudishia kipa wake na akafunga bao la ufunguzi kunako sekunde ya 63.

Juventus walikuwa wametawaliwa kabisa lakini Adrien Rabiot akasukuma shuti la tikitaka na kuokolewa kabla ya Moussa Marega kufunga bao la pili katika sekunde ya 19 ya kipindi cha pili

Lakini Federico Chiesa alifunga bao la kufuta machozi katika dakika ya 82 na kuwapa Juve matumaini katika mchuano wa marudiano wa hatua ya 16 bora mnamo Machi 9.

 

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares