Premier League kuwa na wiki 10 za dirisha la uhamisho wa msimu wa joto kuanzia Julai 27

336
Dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi katika Premier League limekusudiwa kufunguliwa rasmi tarehe 27 ya mwezi wa saba na kutamatika tarehe 5 ya mwezi wa 10 ambapo Shirikisho la Soka duniani Fifa limethibitisha kufunguliwa kwa dirisha hilo la usajili.
Katika hatua nyingine uongozi wa EPL umesema usajili wa ndani utakuwa ukiendelea hata baada ya tarehe ya 5 – 16 ya mwezi Octoba.  “Hakuna usajili wowote ambao unaweza kufanyika katika kipindi hiki hadi tarehe tajwa ndio tunaweza kuanza”.
Premier League haijatangaza tarehe ya kuanza msimu mpya, ijapokuwa vyombo vya habari vinasema huenda ikawa Septemba 12.

Author: Bruce Amani