Prisons, Geita Gold Hakuna Mbabe

30

Tanzania Prisons imetoshana nguvu na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchezo uliopigwa dimba la Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya Leo Alhamis.

Prisons ambao bado hawajakaa eneo nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu walianza kupata bao kupitia kwa Jeremiah Juma kunako dakika ya 38 kabla ya Danny Lyanga kuisawazishia Geita Gold dakika ya 50.

Kwa matokeo hayo, Prisons inafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya 14, wakati Geita Gold pamoja na kufikisha pointi 36 inabaki nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 26.

Author: Asifiwe Mbembela