PSG inaendelea na mazungumzo na Messi

Paris St-Germain iko kwenye mazungumzo na staa wa Argentina Lionel Messi 34, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru kufuatia mkataba wake na Barcelona kufikia tamati ghafla Alhamis wakati anakaribia kumwaga wino wa kutumika Camp Nou.

Kwa sasa wawakilishi wa Messi akiwemo Baba mzazi ambaye ndiye Wakala wako Paris kuangalia uwezekano wa kufanya biashara baina ya klabu hiyo na mchezaji wa kihistoria kutokana na mafanikio binafsi na klabu.

Mbali na mazungumzo ya Jana Ijumaa, Leo Jumamosi Agosti 7, 2021 pia kimefanyika kikao kwa ajili ya kumsajili ambapo imani imeongeza mara dufu kuwa anaweza kwenda Parc Des Princes.

Miaka 21 ya Messi Barcelona ilifika tamati, lakini kesho Jumapili atazungumza na Waandishi wa Habari, akizungumzia tukio hilo Rais wa klabu Joan Laporta amesema kuwa kumbakiza Lionel Messi kungewapa uhatari miaka 50 ijayo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends