PSG wakabidhiwa taji lao la Ligue 1

Paris Saint-Germain wametangazwa kuwa mabingwa watetezi wa Ligue 1 baada ya msimu kusitishwa ukielekea ukingoni kutokana na virusi vya Corona kuingilia kati shughuli hiyo.

PSG wametwaa ubingwa huo wakiwa vinara kwa tofauti ya alama 12 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi kwani ligi hiyo hazijachezwa tangu Marchi 13.

Mapema wiki hii serikali nchini Ufaransa kupitia kwa Waziri Mkuu alisema michezo na mikusanyiko nchini humo haitaendelea mpaka mwezi wa tisa.

Vilabu vilikubaliana kuwa kipindi hiki wameamua kujikita kuwasaidia watu wa afya kupambana na afya zao.

Mwenyekiti wa PSG na Mkurugenzi Mkuu wa timu hiyo Nasser Al-Khelaifi alisema kuwa wafanyakazi muhimu Ufaransa wamejitoa kwa nguvu zao zote kupambana na Corona wanatakiwa kuungwa mkono.

“Tunaunga mkono juhudi za serikali za kumaliza ligi, afya yetu, yao ni kipaumbele chetu cha kwanza”, aliongeza Bosi huyo.

“Kwenye kipindi hiki kigumu, naamini kombe hili litarudisha angalau furaha ya mashabiki wetu, nina furaha kubwa kwani walikuwa na msaada wetu hata katika wakati mgumu tulikuwa pamoja nao”.

Kabla ya serikali kuingilia, Bodi ya uongozi ya liginya Ufaransa ilikuwa imekusudia kurejesha ligi nchini humo Juni 17.

Wakati PSG akitwaa ubingwa wa Ligue 1, Lorient wametwaa taji la Ligue 2 alama moja dhidi ya timu iliyonafasi ya pili lens timu hizo zimefuzu kucheza ligi kuu msimu ujao (Ligue 1).

Amiens na Toulouse zimeshuka daraja kutoka Ligue 1 kwenda Ligue 2.

Ufaransa ligi inafutwa huku bodi ya Uefa ikiwaambia wanachama wake kuwa kutafanyika kikao cha kujadili uwezekano wa kufuta ligi hizo.

Tofauti na kwenye Ligue 1 nchini Uholanzi ligi imefutwa huku kukiwa hakuna timu ya kupanda wala kushuka wakati ligi ya Ubelgiji ligi imefutwa na bingwa kupatikana.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends