PSG yafunga tisa dhidi ya Guingamp, kilio kwa Monaco

Kylian Mbappe na Edinson Cavani walifunga hat-tricks wakati vinara wa Ligue 1 Paris St-Germain walifunga mabao 9 – 0 dhidi ya Guingamp na kupata ushindi wa kuvunja rekodi.

Rekodi hiyo iliishinda iliyowekwa awali na PSG katika uwanja wao wa Parc des Princes wa 8 – 0 dhidi ya Dijon mwaka jana.  Ushindi wao mkubwa zaidi unabaki kuwa 10 – 0 katika Kombe la Ufaransa dhidi ya Cote Chaude mwaka wa 1994. Neymar alifunga mabao mawili, wakai Thomas Meunier akifumania nyavu katika dakika za mwisho mwisho

Siku kumi zilizopita, Guingamp waliwaduwaza PSG kwa kuwazaba 2-1 mjini Paris na kutinga nusu fainali ya Kombe la Ufaransa. PSG ambao wana idadi kubwa kabisa ya mabao 62 katika mechi 19, sasa wako mbele ya nambar mbili Lille na pengo la pointi 13 wakiwa na mechi mbili zaidi za kucheza.

Monaco kilio

Vijana wa Therry Henry Monaco walipewa kipigo kizito hcha 5 – 0 dhidi ya Strasbourg wakati mapambano yao ya kuepuka shoka la kushushwa ngazi yakiendelea kuwa makali hata zaidi na yasiyoweza kufua dafu. Ushindi huo umewaweka Strasbourg katika nafasi ya tano kwenye ligi kuu ya Ufaransa.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends