PSG yaiadhibu Real Madrid Ligi ya Mabingwa

75
Winga wa Kiagentina Angel di Maria ameipatia ushindi PSG dhidi ya Real Madrid klabu aliyowai kuichezea kabla ya kuhamia Manchester United na sasa PSG goli 2 katika ushindi wa 3-0 mashindano ya Ligi ya Mabingwa kundi A.
Goli la Thomas Meunier katika dakika za nyongeza zilipigilia msumari wa moto kwenye kidonda cha kocha Zinedane Zidane “Zizzou” kwani tangu kurejea hali sio shwari huku asilimia ya ushindi ikiwa ni chini asilimia 50 tangu aingia Madrid awamu ya pili.
Angel Di Maria aliyekuwa anafikisha mechi ya 100 kwenye michuano ya Uefa aliweza kutumia vyema usaidizi mzuri wa pasi za Juan Bernat na Idrissa Gana Gueye kufunga magoli ya mepama kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Eden Hazard, alianza kwenye kikosi cha Madrid ikiwa mechi ya pili ya mashindano licha ya kwamba uwepo wake haukusababisha aepuke dhahama ya kipigo kizito kutoka kwa PSG.
Baada ya michezo ya kwenye kundi A kupigwa Jana Real Madrid inakamata nafasi ya mwisho kwenye msimamo huku PSG ikiongoza kwa alama tatu na magoli matatu, Club Br zikiwa na alama moja baada ya mchezo wa kumalizika kwa sare ya 1-1 Brugge na Galatasaray.

Author: Bruce Amani