PSG yaiduwaza Bayern nyumbani, yaichapa 3-2 Ligi ya Mabingwa

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe amefunga goli mbili kwenye ushindi wa goli 3-2 ambao Paris St-Germain wameupata mbele ya mabingwa watetezi Bayern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali raundi ya kwanza.

Mchezo ukikumbushia fainali ya msimu uliopita, PSG ambao wamekuwa hawana bahati pamoja na ujana mwingi kwenye mashindano hayo, wameanza vyema baada ya kupata goli hizo ambazo zinawapa nafasi ya kuingia nusu fainali baada ya mkondo wa pili.

Mshambuliaji Mbappe ilimchukua dakika tatu kufungua akaunti ya magoli baada ya kumalizia vyema mpira wa strika wa Brazil Neymar Jr kabla ya kumshinda kipa Manuel Neuer.

Marquinhos aliongeza bao la pili na kufanya 2-0 lakini goli la mshambuliaji wa Bayern Munich Eric Maxim Choupo-Moting na Thomas Muller kusawazisha ubao na kufanya 2-2 kabla ya kuruhusu bao lingine Bayern kupitia kwa Mbappe tena

Mpaka kipyenga cha mwamuzi kinapulizwa, Bayern Munich wenyeji wa mchezo huo walikuwa 2-3 PSG ukiwa ni mkondo wa kwanza.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares