PSG yaitandika 3-2 RB Leipzig Ligi ya Mabingwa

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi amefunga goli mbili kwenye ushindi wa goli 3-2 walioupata Paris St-Germain dhidi ya RB Leipzig ya Ujerumani kwenye mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Winga wa Kifaransa Kylian Mbappe alikuwa wa kwanza kuandikisha bao la kuongoza kwa upande wa PSG kabla ya Leipzig kuamka kupitia bao la Andre Silva na Nordi Mukiele wote wawili wakimalizia mpira wa krosi wa Angelino

Baadaye nyota Messi alifunga goli moja kabla ya kufunga goli la penati aina ya Panenka na kufanya matokeo kuwa 3-2 ingawa alikuwa kwenye nafasi ya kufunga goli la tatu kufuatia kupata tuta ambalo Mbappe alichukua mpira na kukosa penati.

Unakuwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa PSG kushinda mechi za Uefa hatua ya makundi baada ya awali kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Man City, ambapo sasa wanafikisha pointi saba kileleni mwa Kundi A chini yao ni Manchester City.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends