PSG yaitandika Reims Ligue 1, Messi akicheza kwa mara ya kwanza

Lionel Messi akiingia kwenye dakika ya 66 akitoka mshambuliaji Neymar Jr, matajiri wa Jiji la Paris, Paris St-Germain walishinda bao 2-0 dhidi ya Reims katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa Ligue 1.

Mshambuliaji huyo wa Argentina, akivalia jezi namba 30 kwenye uzi wa PSG alipoingia akacheza kandanda lenye kasi na kusababisha faulo kibao.

Inakuwa klabu ya kwanza kuchezea mbali na Barcelona ambapo alianzia soka la utotoni na ushindani.

“Hajafikia ubora wake, bado hayuko fit asilimia 100”, alisema kocha Mauricio Pochettino.

Kylian Mbappe alifunga magoli yote mawili akitumia vyema pasi ya Angel di Maria na Hakimi Achraf wa Morocco, Mbappe anafunga magoli hayo wakati ambao amekuwa akihusishwa kujiunga na Real Madrid kwa dau la pauni milioni 137 sawa na Euro milioni 160.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares