PSG yakamilisha usajili wa kipa Donnarumma kutoka AC Milan

Paris St-Germain imekamilisha uhamisho wa mlinda mlango wa Italia Gianluigi Donnarumma kama mchezaji huru kutokea AC Milan.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, anajiunga na PSG siku chache baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Euro 2020 katika mchezo wa fainali mbele ya England.
Aliokoa mikwaju ya penati miwili pale ambapo Azzurri walishinda kwa 3-2 baada ya sare ya 1-1 katika dakika 120.
Donnarumma, amemwaga wino wa miaka mitano, anaondoka AC Milan baada ya kandarasi yake kumalizika klabuni hapo.
Donnarumma anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa ndani ya PSG iliyochini ya kocha Mauricio Pochettino baada ya Georginio Wijnaldum, 30, akitokea Liverpool na mlinzi wa kati wa Hispania Sergio Ramos 35, Achraf Hakimi ni mchezaji mwingine ambaye amesinya klabuni hapo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares