PSG yashinda dhidi ya Dortmund

Laana imekwisha. Ile laana iliyokuwa ikiitesa Paris St-Germain ya kutofanya vizuri katika mashindano ya Uefa hatimaye wameimaliza baada ya kubadilisha matokeo kutoka 2-1 mchezo wa kwanza mpaka 3-2 katika mtanange uliopigwa dimba la Parc des Princes dhidi ya Borussia Dortmund.

Katika mtanange ambapo umepigwa bila uwepo wa mashabiki kutokana na hofu ya Virusi vya Corona, staa wa timu hiyo Neymar alianza kufunga goli la kwanza kwa kichwa kabla ya Juan Bernat kufunga goli la pili akimalizia pasi ya Pablo Sarabia.

Mbali na kufungwa, Dortmund watajilaumu wenyewe baada ya kupoteza nafasi nyingi za wazi hata hivyo kiungo wao Emre Can alionyeshwa kadi nyekundu na kufuta matumaini ya kushinda mchezo huo.

Katika jambo la kuvutia baada ya mchezo huo kumalizika, wachezaji wa PSG walijumuika na mashabiki waliojitokeza na kuwasubili nje ya uwanja wa Parc des Princes kushangilia ushindi huo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends