PSG yashinda kibabe, Neymar alimwa kadi nyekundu

51

Staa wa Paris Saint Germain Neymar ameonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligue 1 ambapo PSG walikuwa wametoka nyuma na kushinda goli 4-3 dhidi ya Bordeaux.

Ushindi wa PSG unawafanya kurudi katika njia ya ushindi kufuatia matokeo mawili mfululizo yasiyo ya alama tatu, sare ya goli 4-4 dhidi ya Amiens wiki iliyopita na ikapoteza 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo pia waliianzia nyuma kwa goli la mapema la Hwang Ui-jo dakika ya 18.

Mshambuliaji Edinson Cavani alianza kufungua akaunti ya goli kabla ya mlinzi wa Kibrazil Marquinhos kupata goli la pili kwa PSG ambapo wakati mchezo unaelekea mapumziko Pablo aliipa matumaini mapya Bordeaux baada ya kufunga goli na kufanya mpira kwenda mapumziko matokeo yakiwa 2-2.

Marquinhos na Kylian Mbappe walifunga goli mapema kipindi cha pili kabla ya Ruben Pardo kufunga na kuipa hali ya kupambana zaidi Bordeaux ambao wanakamata nafasi ya

Neymar alionyeshwa kadi ya njano ya pili baada ya kumpa changamoto kubwa Yacine Adli, kadi nyekundu itamfanya akose mchezo wa nyumbani dhidi ya Dijon, huku ikiwa ni kadi ya pili tangu aonyeshwe nyekundu mwezi Octoba mwaka 2017.

Alama tatu za PSG zinaifanya kurudisha mwanya wa alama 13 dhidi ya timu ambayo inakamata nafasi ya pili Marseille ambao nao walipigwa 3-1 na Nantes.

Author: Bruce Amani