Pulisic aipa Chelsea bao la ugenini katika sare ya 1-1 dhidi ya Real Madrid

Real Madrid wamelazimishwa sare ya goli 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali mchezo uliopigwa dimba la Alfredo de Stefano nchini Hispania ukiwa mkondo wa kwanza ambapo marudiano itakuwa wiki lijalo.

Madrid ambao walikuwa wanamkosa nahodha wake Sergio Ramos kutokana na majeruhi ambayo aliyapata wiki tatu nyuma walikuwa nyuma kwa kipindi kirefu mpaka pale walipogungwa goli.

Bao la Chelsea limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic akimalizia pasi ndefu ya beki wa katikati ya Antonio Rudiger ungwe ya kwanza.

Karim Benzema alikwamisha mpira nyavuni likiwa ni bao la kusawazisha la aina yake ukiwa ni mpira uliotokana na kona.

Hata hivyo, habari njema ni kurejea kwa winga wa Ubeligiji Eden Hazard ambaye alipata dakika chache kwenye mechi hiyo baada ya kuwa nje ya uwanja tangia mwezi Januari 30.

Mkondo wa pili, Chelsea wanahitaji sare tasa kusonga mbele au ushindi wa aina ile kutinga hatua ya fainali ya Uefa kwa mara ya kwanza chini Thomas Tuchel.

Kesho Jumatano, ni nusu fainali ya pili ya Uefa baina ya Paris St-Germain dhidi ya Manchester City.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares