Rafael Nadal atinga robo fainali ya fainali ya ATP London

Rafael Nadal amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya fainali za ATP kwa kumbwaga mshindi wa Kombe hilo mwaka 2019 Stefanos Tsitsipas kwa seti tatu.

Nadal ambaye ni raia wa Hispania anashikilia namba mbili kwenye orodha ya wanatenis bora duniani alimfunga Tsktsipas raia wa Ugiriki kwa seti za 6-4 4-6 6-2 kwenye mchezo uliopigwa London Jana Alhamis.

Rafael Nadal, 34, aliutawala mchezo hadi pale ambapo alipopoteza seti ya pili na kurudi tena kwa kishindo kumaliza mchezo.

Mshindi huyo wa mataji 20 ya Grand Slam atakutana na Daniil Madvedev raia wa Urusi kwenye mechi ya nusu fainali kwenye uwanja wa O2 kesho Jumamosi.

Mapema siku ya Alhamis, Dominic Thiem alipoteza seti 6-2 7-5 kwa Mrusi Andrey Rublev.

Thiem ambaye ni mshindi wa US Open alifika hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Nadal na Tsitsipas na kushinda Group London 2020.

Author: Bruce Amani