Raia wa kigeni wahusishwa na utekwaji wa “Mo”

120

Kufuatia habari za kutekwa  kwa mfanyabishara maarufu nchini Tanzania ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji) alfajiri ya leo, Oktoba 12, 2018,  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema katika taarifa ya awali kuwa, watu waliohusika na utekaji huo wawili kati yao ni wa kigeni “wazungu”.

Mambosasa amesema kwamba wakati Dewji anafika kwenye gym ya Colosseum eneo la Oyster Bay jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi, kulikuwa na gari moja lililokuwa limefika hapo kabla na kuegeshwa mbele yake na jingine lilikuwa nje.

Mambosasa  ameeleza kwamba gari lililokuwa ndani liliashiria kwa kuwasha taa, na lililokuwa nje likaingia ndani na kuegesha mbele ya gari la Dewji ambapo walitoka Wazungu wawili wakaambatana na Dewji na kumuingiza kwenye gari lao aina ya Toyota Surf na kuondoka naye kuelekea maeneo ya Masaki.

Author: Master Tindwa