Rais wa CAF aachiwa huru bila kufunguliwa mashitaka

Rais wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF Ahmad Ahmad ameachiwa huru bila ya kufunguliwa mashitaka hii leo, ikiwa ni skiku moja baada ya kukamatwa kwa ajili ya kuhojiwa mjini Marseille nchini Ufaransa.

Mwendesha mashitaka wa umma mjini humo, Xavier Tarabeux, amesema Ahmad, aliyekuwa nchini Ufaransa kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, uliofanyika siku ya Jumatano. Ahmad alikamatwa na kuhojiwa, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa ufisadi, kuvunja imani na kughushi.

Author: Bruce Amani