Rais wa CAF akamatwa na kuhojiwa na maafisa wa Ufaransa

Makamo mwenyekiti wa shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA, Ahmad Ahmad anazuwiliwa na kuhojiwa na maafisa wa Ufaransa katika kadhia ya madai ya uhalifu dhidi ya taasisi hiyo ya soka la kimataifa.

Kisa hicho kinajiri siku moja kabla ya fainali za kombe la dimba la wanawake kuanza mjini Paris. “Ahmad Ahmad anahojiwa na maafisa wa Ufaransa kuhusiana na madai yanayohusiana na mhula wake kama mwenyekiti wa shirikisho la kabumbu barani Afrika – shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIA limesema katika taarifa yake.

FIFA linasema halijui “undani” wa uchunguzi huo na kwa namna hiyo haliwezi kutoa maelezo yoyote. Shirikisho la dimba ulimwrenguni FIFA limewataka maafisa wa Ufaransa liwapatie “maelezo yoyote yanahitaji kushughulikiwa na ” tume ya maadili” ya FIFA.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends