Rais wa CAF kutua Tanzania kuziangalia Yanga na Simba

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mchezo wa ‘watani wa jadi’ kati ya Yanga na Simba mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, Machi 8, 2020.
Kiongozi huyo atafanya ziara ya siku tatu hapa nchini, itakayoanza Machi 7 hadi Machi 10, ambapo katika ziara yake hiyo, Machi 8, atakuwepo kwenye mechi ya watani wa jadi Yanga Vs Simba akiwa ni mgeni rasmi.
Katika ziara hiyo, pia Ahmad Ahmad atakutana na viongozi mbalimbali wa serikali kuzungumzia maendeleo ya mpira hapa nchini kwa utaratibu utakaopangwa na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Ahmad Ahmad amekuwa na utaratibu wa kutembelea mashirikisho mbalimbali ya soka yaliyo chini yake, ambapo mara ya mwisho kuja hapa nchini ni Februari 22, 2018 alipoambatana na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends