Rais wa Fifa Infantino aipongeza Simba kuwa Mabingwa VPL 2020/21

Rais wa Shirikisho la Kandanda duniani Fifa Gianni Infantino ameipongeza klabu ya Simba kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu wa 2020/21 ikiwa ni mara ya nne kufanya hivyo.

 

Katika barua yake ya pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia, Rais Infantino amesema ubingwa wa Simba ni matokeo ya juhudi na utekelezaji wa majukumu kwa kila mmoja ndani ya klabu hiyo.

 

Aidha, Rais Infantino amempongeza Karia kwa kuendelea kusimamia weredi wa michezo nchini Tanzania.

 

Klabu ya Simba ilifanikiwa kutawazwa Mabingwa wa VPL Julai 11 kwa kuifunga bao 2-0 Coastal Union na kufikisha alama ambazo zisingeweza kufikiwa na klabu yoyote hata kabla ya michezo miwili.

 

Ubingwa huo unakuwa wa nne mfululizo kwa Wekundu wa Msimbazi Simba wakivunja rekodi ya Yanga ya kubeba taji mara tatu mtawalia.

 

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares