Rais wa La Liga nchini Hispania awapinga wanaofuta ligi barani Ulaya

Rais wa ligi kuu ya Hispania La Liga Javier Tebas amesema haelewi kinachoendelea hivi sasa kutokana na mataifa jirani barani Ulaya kuanza kuchukua hatua ya kufuta ligi zao.

Rais huyo ameyasema hayo leo baada ya kupokea taarifa kuwa ligi ya Ufaransa imefutwa rasmi kufuatia tamko la Waziri Mkuu wa Ufaransa kutangaza mikusanyiko yote kurejea mwezi wa tisa jambo lililochukuliwa kuwa vigumu ligi kuendelea mwezi Septemba kwa sababu kinakuwa ni kipindi cha msimu mpya.

“Sielewi kabisa kwa nini iwe vigumu kucheza mechi bila mashabiki, huku tukichukua tahadhari zote za wataalamu, kuliko kuchukua maamuzi yanayofanana yaani ni kama tunavua samaki ndani ya boti la uvuvi”.

“Kama ni masuala ya kuimarisha uchumi ni ngumu kulisemea lakini tunaweza kujitunza na kufuata kanuni zote kuliko msimu kuishia njiani. Kwenye baadhi ya mataifa tumeona wakiruhusu wachezaji kurejea mazoezi (Ujerumani, Italia) nadhani huo ndio mfano wa kuingwa na sio kufuta,” amesema Rais Tebas.

Aidha, amesisitiza kuwa nchini Hispania mpira wa miguu ni muhimili wa uchumi hivyo watachukua kila hatua, watafanya kila njia kuhakikisha ligi inachezwa na kumalizika.

Hispania, Italia, China na Marekani ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na athari kubwa za virusi vya Corona.

Tayari Uholanzi ligi ilishafutwa, Ubeligiji pia kimebaki kikao kimoja kufanya maamuzi kama hayo, ambapo Uefa wameshatoa uhuru kuwa endapo ligi haitamalizika Shirikisho la nchi husika litachagua timu za kushiriki kwenye mashindano ya Uefa msimu ujao.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends