Rais wa Olimpiki asema hukumu dhidi ya Semenya inakanganya

Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC Thomas Bach ameitaja hukumu dhidi ya shauri la mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya, kuwa ni ya kukanganya.

Bach anasema kamati ya wataalamu itapitia hukumu hiyo na kuangalia utekelezaji wake.

Semenya, mshindi mara mbili wa mbio za Olimpiki alishindwa katika rufaa yake dhidi ya IAAF ya kuhusu sheria za kudhibiti homoni ya kiume katika wanariadha wa kike wanaoshiriki kwenye mbio fupi.

Hukumu hiyo imezusha mjadala katika jumuiya ya kimataifa ambapo Umoja wa Mataifa ulionya kwamba michezo sasa imekuwa sehemu ya kuigawa jamii kwa misingi ya kijinsia.

Author: Bruce Amani