Rais wa Real Madrid Perez asema hakuna timu iliyojitoa European Super League, ni hofu tu

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema timu 12 zilizokubali kujiunga na Ligi mpya ya European Super League haziwezi kujiondoa kutokana na kuingia mkataba maalumu na ya kisheria ya kuwa washirika.

Vilabu tisa kati ya 12, ukijumulisha vyote sita vya England vilitangaza kujitoa siku ya Jumanne baada ya mpango huo kupigwa vitisho na Shirikisho la Kandanda Ulaya – Uefa na Shirikisho la Soka Duniani – Fifa.

Real Madrid, Barcelona na Juventus bado havijatangaza kujitoa.

“Sihitaji kuelezea mkataba tulioingia una maana gani, lakini hakuna klabu ambayo inaweza kujiweka kando na michuano hii baada ya mkataba ule”, alisema Perez ambaye yuko mbele sana kutetea ujio mpya wa Ligi hiyo.

“Baadhi ya vilabu vimejitoa kutokana na presha, nina imani kuwa mpango huu utaendelea siku si nyingi”, ameongeza Perez.

Hata hivyo, Rais Perez amekanusha taarifa zinazosema kuwa kujiweka kando kwa vilabu tisa ni kutokana na benki ilidhamini ujio wa ligi hiyo kutoka Marekani kuondoa udhamini wao wa zaidi ya Euro bilioni 3.5.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares