Rais wa soka wa Ujerumani Fritz Keller asema anazifahamu kwa sehemu tu hatua za kudhibiti virusi vya corona

76

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Ujerumani DFB Fritz Keller leo hii ameliambia gazeti la Bild am Sonntag kwamba anazifahamu kwa sehemu tu hatua za kukabiliana na kuenea kwa maambukizi ya corona. Na kuongeza kusema katika soka, hatari ya kuambukizwa uwanjani inaonekana kwa kiwango kidogo tu.

Hata hivyo alisema ni vyema kuwazuia watoto kutokwenda kufanya mazoezi ya soka katika kipindi hiki. Hata hivyo Keller alisema masomo ya chekechea yataendelea kuwa wazi, na hata hivyo watoto watapaswa kusalia madarasani.

Kwa mwezi huu, Novemba serikali ya Ujerumani imechukua hatua kali zenye kugusa moja kwa moja maisha ya umma kwa lengo la kudhibiti kasi ya maambukizi ya virusi vya corona. Lakini soka la kulipwa, kama ligi ya Ujerumani Bundesliga na ligi ya daraja la pili inaweza kuendelea pasipo mahudhurio ya watu. Na michezo isiyo ya kulipwa lazima isitishwe kabisa kuanzia kesho Jumatatu.

Author: Bruce Amani