Rais wa Uefa Aleksander Ceferin kupeleka Kombe la UCL na Europa Uwanjani

Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya Aleksander Ceferin atakuwa na hotuba fupi katika mchezo wa fainali za michuano ya ulaya msimu huu (Europa Ligi na UCL) ambapo atatumia muda huo kupeleka pia Kombe la fainali husika.

Ceferin atafanyiwa vipimo vya Virusi vya Corona siku mbili kabla mchezo wa fainali na hatalazimika kuvaa barakoa katika kipindi ambacho anaingia kuwasilisha hotuba na kombe lenyewe.

Rais huyo amesema ataufanya uwasilishaji wa hotuba hizo kuwa fupi na ya kuvutia licha ya fainali zote kuchezwa bila uwepo wa mashabiki.

Mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa utachezwa Agosti 23 mjini Lisbon, siku mbili bada ya kuchezwa fainali ya ligi ya Europa mjini Cologne

Michuano yote kuanzia raundi ya nane imechezwa kwa mkondo mmoja ikiwa ni sehemu ya madhara yaliyojitokeza kutokana na virusi vya Corona.

Maamuzi ya Ceferin ya kuwasilisha hotuba yametofautiana na mfumo ambao Chama cha Soka England kilitumia kukabidhi taji la FA Agosti 1 kwani Kombe liliachwa na mchezaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Author: Asifiwe Mbembela