Rais wa zamani Real Madrid afariki kwa Corona

Rais wa zamani wa Real Madrid Lorenzo Sanz amefariki dunia baada ya kulazwa Jumamosi kutokana na virusi vya Corona.

Sanz, 76, alikuwa Rais wa Madrid kuanzia mwaka 1995-2000, kipindi ambacho Real walitwaa ubingwa mara mbili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uefa.

“Baba yangu hatunae tena, amefariki” aliandika mtoto wa kiume wa Sanz, Lorenzo Sanz Duran kwenye mtandao wa Twitter.

Katika uongozi wake Sanz aliwasajili wachezaji kama Roberto Carlos, Clarence Seedorf na Davor Suke.

Mwaka 2000 aliangushwa na Rais wa sasa katika uchaguzi wa klabu hiyo, Perez aliiegeuza Madrid kuwa timu ya Galatico akiamini katika matumizi makubwa ya fedha kwenye usajili.

Mtoto wake Sanz, Fernando, 46, aliichezea pia Real Madrid kuanzia 1996-1999 kabla ya kumalizia kandanda yake Malaga.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments