Rais wa zamani wa Uefa Michel Platini akamatwa Ufaransa

Rais wa wa zamani wa Shirikisho la Soka Ulaya – UEFA Michel Platini anahojiwa na polisi baada ya kukamatwa katika uchunguzi wa rushwa kuhusu kura iliyoipa Qatar fursa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022. Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa mahakama aliyekataa kutajwa kwa majina.

Akithibitisha ripoti hizo zilizochapishwa na tovuti ya habari ya mtandaoni ya Mediapart, afisa huyo amesema Platini alikamatwa leo asubuhi  wakati alipoitwa katika Ofisi ya Kupambana na Rushwa ya Polisi ya Mahakama nje ya mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Baada ya kuhojiwa na polisi, Platini ambaye ni mchezaji maarufu wa zamani wa Ufaransa, anaweza kuachiliwa huru au kufunguliwa mashtaka rasmi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends