Raja wamteuwa Patrice Carteron kuwa kocha wao mpya

Mabingwa watetezi wa taji la Shirikisho barani Afrika, Raja Casablanca wa Morocco, wamemteua Mfaransa Patrice Carteron kuwa kocha wao mpya. Carteron mwenye umri wa miaka 48, anachukua nafasi ya Mhispania Juan Carols Garrido ambaye mkataba wake ulimalizika siku ya Jumatatu wiki hii.

Kocha huyo ametia saini kuifunza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu, huku akiwa na uhuru wa kuendelea kuifunza klabu hiyo. Kabla ya kupewa kazi katika klabu hiyo, kocha huyo amewahi kuifunza klabu ya TP Mazembe ya DRC, Al Ahly ya Misri na timu ya taifa ya Mali.

Kazi kubwa iliyo mbele ya kocha huyu mpya, ni kuisaidia Raja Casablanca kutetea taji lake na imepangwa katika kundi la A na Hassania Agadir na RS Berkane zote kutoka Morocco na AS Otono ya Congo Brazaville.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments