Ramos arejea kuipa nguvu Real Madrid mbele ya Chelsea Ligi ya Mabingwa Ulaya

Nahodha wa kikosi cha Real Madrid Sergio Ramos yuko fiti kuwakabili Chelsea katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaopigwa dimba la Stamford Bridge Jumatano Mei 5.

Ramos, 35, hajacheza mechi yoyote tangia mwezi Machi kufuatia kupata majeruhi ya kifundo cha mguu lakini hata hivyo kocha Zinedine Zidane amesema Ramos amepona na yuko na timu.

Los Blancos wanafukuzia taji la 14 la Ligi ya Mabingwa Ulaya, na fainali ya kwanza tangia mwaka 2018.

Kwa upande wa Chelsea, mlinzi wa kati raia wa Ujerumani Antonio Rudiger yuko nusu kwa nusu kucheza mechi hiyo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares