Ramos kuikosa Liverpool Ligi ya Mabingwa Ulaya

Mlinzi mahiri na nahodha wa kikosi cha Real Madrid Sergio Ramos ataikosa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali ya Uefa dhidi ya Liverpool kufuatia kupata majeruhi ya msuli.

Ramos mwenye umri wa miaka 35 aliyapata majeruhi hayo kwenye mechi ya timu ya taifa ya Hispania na hivyo atakosa mechi za raundi zote mbili.

Real Madrid watacheza na Liverpool Jumanne Aprili 6 na Jumatano ya Aprili 14 itacheza dhidi ya Barcelona katika mtanange wa El Clasico wa La Liga.

Ramos alisema alitambua hayuko sawa akifanya mazoezi ya mwisho kuelekea mbilinge yao dhidi ya Kosovo ambapo Hispania ilishinda bao 3-1.

Real watakuwa nyumbani mchezo wa kwanza kabla ya kusafiri kwenda Anfield.

Bila shaka itakuwa siku nzuri na taarifa nzuri kwa Liverpool na mashabiki wa klabu hiyo hasa baada ya tukio lake la mwaka 2018 kwa Mohammed Salah.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares