Rangnick, mrithi wa muda wa Solskjaer Man United

Manchester United imefikia maamuzi ya kumteua kocha Ralf Rangnick kuwa kocha wao wa muda kwa mkataba wa miezi sita kurithi mikoba ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63, raia wa Ujerumani atajiunga na kikosi cha Manchester United kuanzia wiki lijalo kipindi chote hichi United watakuwa wanaendelea kutafuta kibali cha kazi kwa kocha huyo wa zamani wa Schalke 04 ya Ujerumani.

Rangnick anaelekea kutangazwa United baada ya Solskjaer kufukuzwa kazi hata hivyo, bado makubaliano baina ya Mwalimu huyo mkongwe na sasa Mkurugenzi wa Michezo katika klabu ya Lokomotiv Moscow na United hayajafikiwa.

Rangnick ni moja ya makocha wenye wasifu wa kawaida kwa kufundisha klabu za kawaida, hata mafanikio yake ni ya kati pia, mathalani mwaka 2018 akiwa Schalke 04 alibeba taji la ubingwa wa Kombe la Ujerumani ambapo mwaka 2019 aliifikisha fainali klabu ya RB Leipzig.

Hata hivyo, kocha wa muda (dharura) Michael Carrick ambaye alikuwa msaidizi wa Solskjaer atakalia kiti cha ukocha kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea Jumapili Novemba 28 Stamford Bridge.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends