Rashford aipa England ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Romania

Kikosi cha taifa cha England kimemaliza michezo ya kupasha misuli kuelekea michuano ya Euro 2020 kwa ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi Romania mtanange uliopigwa dimba la Riverside.
England ikiwa ni miongoni mwa timu zinazopewa kipaumbele cha kutwaa taji hilo chini ya kocha Gareth Southgate kwa mara nyingine tena alianzisha kikosi cha wachezaji ambao hawana uhakika wa namba ya moja kwa moja kama Ben Godfrey, Ben White na James Ward-Prowse.
Ubora mkubwa wa kiungo mshambuliaji wa Aston Villa Jack Grealish umeendelea kudhihirisha umuhimu kwa timu hiyo baada kuwa kwenye ubora kabla ya kusababisha penati iliyopigwa na nahodha Marcus Rashford.
Lilikuwa tukio kubwa kwa Rashford kufunga goli hilo huku akiwa na kitambaa cha unahodha, kwa sababu anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuvalia kitambaa akiwa na umri wa miaka 23 na siku 218.
England walipoteza nafasi za uongozi imara zaidi kufuatia kiungo mkabaji wa Liverpool Jordan Henderson kukosa penati baada ya mshambuliaji wa Everton Calvert Lewin kufanyiwa madhambi.
Baada ya mchezo huo, kocha Southgate anaanza rasmi mikakati kuelekea Juni 13 ambapo timu yake itashuka dimbani kumenyana vikali dhidi ya wanafainali wa Kombe la Dunia mwaka 2018 Croatia.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares