Rashford ampa maumivu kocha Ole Gunnar Solskjaer Man United

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema atazungumza na wataalamu wa afya kujua kama mshambuliaji wake Marcus Rashford anahitaji kufanyiwa upasuaji au anaweza kuendelea na kandanda akiwa hivyo.

 

Strika Rashford alikutana na wataalamu wiki iliyopita kuhisi kuwa pengine kufanyiwa oparesheni ni njia pekee ambayo inaweza kumuondolea maumivu ya bega ambayo yamemsumbua kwa miezi saba.

 

Hata hivyo, kutokana na kauli ya kocha Solskjaer na jopo lake inaonekana wazi kuwa bado hakuna imani ya wataalamu wa timu ya taifa ya England ambao walimfanyia uchunguzi wa awali na kubaini kuwa kuna tatizo.

 

Akizungumza baada ya mechi ya kujiandaa na msimu ujao iliyopigwa Leo Jumapili Julai 18 ambapo Manchester United imeshinda bao 2-1 dhidi ya Derby County, Solskjaer amesema maamuzi mwisho “nasubilia yachukuliwe”.

 

“Tunatakiwa kuchukua hatua sahihi kwa Marcus, na klabu pia. Tunahitaji kuliangalia vyema na wataalamu wangi”.

 

Goli la Tahith Chong, ambaye atakuwa na Birmingham kwa mkopo, pamoja na Facundo Pellistri, 19, wa Uruguayi wote walifunga goli wakati la kufutia machozi kwa Derby County likifungwa na Colin Kazim-Richards.

 

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares