Rashford fiti kuwavaa Granada Ligi ya Europa

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford yuko fiti kuwakabili Granada mchezo wa Ligi ya Europa hatua ya robo fainali utakaopigwa dimba la Sevilla mkondo wa kwanza.

Rashford, 23, alifunga goli moja katika ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Brighton wikiendi iliyopita hata hivyo hakumaliza dakika 90 baada ya kufanyiwa faulo mbaya na mchezaji wa Brighton.

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England amesafiri pamoja na kikosi kizima cha Manchester United kwenda Hispania.

“Bado hatujafanya maamuzi kama ataanza au ataanzia bechi”, alisema kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Mbali na wachezaji wengine, Man United wamesafari na Juan Mata, Amad Diallo na kinda Anthony Elanga.

Anthony Martial hatakuwa sehemu ya kikosi cha Manchester United kutokana na majeruhi ya goti wakati Eric Bailly akikosa kutokana na kuwa chanya wa Covid-19.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares