Ratiba ya msimu mpya wa kandanda Kenya yatolewa

Kampuni inayosimamia ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL, tayari imetangaza kuanza kwa msimu mpya wa ligi nchini humo. Kwa mara ya kwanza, ligi itaanza mwezi Desemba na sio Februari kam ilivyokuwa desturi.

Msimu mpya utaanza tarehe nane mwezi Disemba ambapo mabingwa watetezi Gor Mahia wataanza harakati za kutetea taji lao dhidi ya Bandari FC ya Mombasa, iliyomaliza katika nafasi ya pili msimu huu.

Disemba 8

Nakumatt/Ushuru vs Sofapaka (Ruaraka)
Mathare vs Chemelil (Kasarani)
Bandari vs Gor Mahia (Mbaraki)
Leopards vs Sharks (Machakos0
Homeboyz vs KCB (Bukhungu)
Posta vs Western Stima (Ruaraka)

Disemba 9

Zoo vs Nzoia Sugar (Kericho)
Sony vs Tusker (Awendo)
Vihiga vs Ulinzi Stars (Mumias)

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends