Raundi ya 16 bora Champions League kurudi kibabe, Liverpool mdomoni mwa RB Leipzig, PSG ugenini kwa Barca

Hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inarejea tena Leo Jumanne baada ya kusimama kwa takribani miezi mitatu kwa klabu zilizoingia kupepetana vikali kuingia hatua ya robo fainali, nusu na hatimaye fainali na kuwa bingwa.

Licha ya kurejea kwa mashindano hayo bado changamoto kubwa ni janga la Covid-19 ambalo linafanya baadhi ya mechi kuhamishiwa viwanja huru kutokana na vizuizi ambavyo baadhi ya mataifa imeviweka kama Ujerumani na Hispania.

Kutokana na vizuizi hivyo, mechi mbalimbali zimehamishwa ili tu zimalizike na kumpa bingwa kuanzia Uefa na Ligi ya Europa.

Mechi ambazo zitapigwa leo Uefa ni matajiri wa Jiji la Paris, Paris St Germain dhidi ya Barcelona katika mchezo utakaopigwa dimba la Camp Nou kuanzia majira ya saa tano kamili usiku.

Mechi nyingine ni ile ya Liverpool dhidi ya RB Leipzig, mtanange ambao utachezwa uwanja huru Jiji la Budapest nchini Hungary kutokana na athari ya Covid-19 nchini Ujerumani pamoja na vizuizi vya hapa na pale.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares