RB Leipzig yatinga fainali Kombe la Ujerumani kwa kuivunja moyo Werder Bremen na bao la jioni

Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amekiongoza kikosi hicho kufika fainali ya Kombe la Ujerumani – DFB Pokal baada ya kushinda kibabe goli 2-1 dhidi ya Werder Bremen mtanange uliopigwa Ijumaa Aprili 30.

Anaifikisha fainali wakati tayari, mwishoni mwa msimu huu ataondoka klabuni hapo na kujiunga na Bayern Munich akirithi mikoba ya Hans Flick aliyeomba kuondoka kutafuta changamoto mpya.

Goli la Emil Forsberg lililofungwa kwenye muda wa ziada dakika ya mwisho kabisa ya 121 lilitosha kuwapa ushindi Leipzig ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga.

Katika dakika 90, timu zote hazikufungana ingawa dakika za ziada zilifanya bao la Forsberg kuwa la 2-1 baada ya magoli mengine kufungwa awali.

Lakini kabla ya hapo, Hwang Hee-chan aliwapa uongozi Leipzig bao lililosawazishwa na Leonardo Bittencourt katika kipindi cha kwanza cha dakika za nyongeza.

Kwingineko, Borussia Dortmund watacheza dhidi ya timu ya daraja la pili Holstein Kiel katika nusu fainali ya pili itakayopigwa Leo Jumamosi.

Fainali ya Kombe la Ujerumani itapigwa Mei 13.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares