Juventus yanyemelea taji la 9 mfululizo kwa kuichapa Inter Milan

Bila uwepo wa mashabiki katika uwanja wa Allianz kutokana na hofu ya Virusi vya Corona, Juventus imeichapa Inter Milan 2-0 na kupanda mpaka nafasi ya kwanza katika Seria A kwa kuishusha Lazio.

Ukiwa mchezo wa dabi na wenye kuvuta hisia za mashabiki umechezwa bila mashabiki kufuatia katazo cha chama cha michezo nchini humo kutoruhusu mikusanyiko ya watu katika viwanja vya michezo na sehemu nyingine mpaka April 4 ambapo huenda wakaanza kutoa ruhusa.

Watu 366 wameshafariki nchini Italia kutokana na ugonjwa huo wakati watu 7375 wakiwa wameathirika na Virusi hivyo hatari vya Corona.

Ushindi wa Vibibi kizee vya Turin ulipitia kwa Aaron Ramsey na Paulo Dybala na sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama moja na Lazio.

Ushindi wa Juve unahitimisha mbio za ubingwa za Inter Milan kwani wanakamata nafasi ya sita alama tisa chini ya kinara Juventus.

Cristiano Ronaldo ameshindwa kuendeleza rekodi yake ya ufungaji katika michezo 11 imefikia tamati jana ambapo aliishia kutoa asisti badala ya kuendeleza rekodi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Gabriel Batistuta na Fabio Quagliarella.

Inakuwa mara ya kwanza Ronaldo kutofunga goli katika michezo ya Seria A tangu alipofanya hivyo Novemba 10.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends