Majeruhi yamuondoa Maddison timu ya taifa ya England

Kiungo mshambuliaji wa Leicester City na timu ya taifa ya England James Maddison amejiondoa kwenye kambi ya timu ya taifa kutokana na maradhi aliyoyapata akikitumikia kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu Euro 2020.

Madison, 22, yupo kwenye kiwango cha juu tangu aibuke Leicester ambapo amefunga goli 3 msimu huu, licha ya kwamba hajacheza mchezo wowote ndani ya Three Lions.
Safari ya kufuzu inanukia kwa England kwani endapo itapata ushindi dhidi ya Jamuhuri ya Czech siku ya Ijumaa watakuwa wamejikatia tiketi ya kushiriki michuano hiyo mwaka 2020.
Maddison anakuwa mchezaji wa tatu kujiondoa kwenye kikosi hicho baada ya Fabian Delph na Tom Heaton wote kutokana na majeruhi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends