Tetesi za Usajili: Willian aomba kuhama Chelsea, David Alaba ahusishwa na Madrid na Barcelona

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News itakuwa inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya.

Manchester United huenda wakamalizana na Nemanja Matic leo kwa kumpa kandarasi ya miaka miwili yenye thamani ya mshahara wa pauni 140, 000 kwa wiki, gazeti la Sun limeripoti.

Mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, ametoa vifaa 50 kwa viongozi wa NHS kwa ajili ya kuendelea kupambana na Corona katika hospitali ya London, gazeti la Times limeripoti.

Straika wa West Brom Charlie Austin amesema haitakiwi watu kuuchukulia ugonjwa wa Corona kiurahisi kwani ndiyo sababu iliyopelekea kukutwa na virusi hivyo, limeripoti gazeti la Telegraph.

Winga wa Chelsea Willian, 31, ameiomba klabu yake kumuachia hur

u na kwenda kujiunga na timu ya nyumbani kwao Brazil ambayo alitokea, limeripoti gazeti la Mirror.

Liverpool wapo katika meza ya makubaliano juu ya kumsainisha kiungo wa Lille na taifa la Ufaransa Boubakary Soumare, 21, gazeti la Sport limeripoti.

Winga wa Sassuolo Jeremie Boga, 23, huenda akarejea darajani Stamford Bridge kutoka na kipengele cha mauzo kufikiwa cha paundi milioni 12.8, gazeti la Mail limetoa taarifa hiyo.

Juventus wanahitaji kumtumia kiungo wa Bosnia-Herzegovina Mirelem Pjanic kama chambo ya kuishawishi Chelsea kumwachia kiungo wao mkabaji Jorginho kwenda Turin, gazeti la Corriere dello Sport.

Mchezaji aliye kwa mkopo Manchester United Odion Ighalo, 30, hupata paundi 8000 kila akifunga goli na paundi 9000 kama timu hiyo ikishinda mbali na mshahara wake wa paundi 180,000 limeripoti gazeti la Sun.

Barcelona na Real Madrid ziko vitani kuwania mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, 27, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni huku kukiwa hakuna uhakika kama ataongeza mkataba mpya Allianz Arena, gazeti la Bild la Ujerumani limeripoti.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments