Real Madrid wafadhaishwa na bao la dakika ya mwisho la Valladolid

Real Madrid wamebaki kujikuna vichwa baada ya Valladolid kusawazisha zikiwa zimesalia dakika mbili tu mechi kukamilika katika La Liga.

Sergi Guardiola ndiye aliyesababisha maangamizi hayo kwa kufunga bao safi alipompiga chobo kipa wa Real Thibaut Courtois.

Mfaransa Karim Benzema aifikiri ameipa Real ushindi katika dakika ya 82 baada ya kugeuka kwa kasi na kusukuma wavuni mpira.

Real aliingia katika mechi hii ya pili ya msimu baada ya kuwafunga Celta Vigo 3 – 1 katika mechi yao ya ufunguzi huku Gareth Bale kwa mara nyingine akipewa katika kikosi cha kwanza

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends