Real Madrid wafuzu 16 bora Ligi ya Mabingwa kwa kuwanyamazisha Sheriff

Real Madrid imefanikiwa kuibuka na ushindi na kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora kufuatia matokeo ya bao 3-0 dhidi ya Sheriff Tiraspolya Moldova. Baada ya kufuzu, Real Madrid unakuwa mwaka wa 25 mfululizo kucheza hatua ya mtoano ambapo hata Sheriff hawakuonekana wakitoa ushindi wa kujitosheleza.

Mabao ya Real Madrid yakifungwa na mlinzi wa zamani wa Bayern Munich David Alaba, Toni Kroos kabla ya mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo Karim Benzema kutupia la tatu. Matokeo hayo yanaifanya Real Madrid kutinga 16 bora huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi, mchezo mwingine katika kundi hilo Inter Milan wameichapa Shakhtar Donetsk 2-0.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends