Real Madrid wapoteza nafasi ya kukamata usukani

50

Real Madrid ilitupa nafasi ya kuchukua usukani wa La Liga baada ya wapinzani wao wakuu Barcelona na Atletico Madrid kuteleza. Madrid waliambulia sare ya 0 – 0 nyumbani dhidi ya Real Betis katika Jumamosi iliyokuwa ngumu kwa timu hizo tatu kuu za Uhispania.

Real walikuwa na msisimko mkubwa kabla ya mechi baada ya kuwachabanga Leganes 5 – 0 katikati mwa wiki na walianza mechi ya jana kwa kasi na kuonekena kupata bao la mapema kupitia Eden Hazard. Lakini bao hilo likafutwa na VAR kwa sababu ya kuotea.

Real wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, na pointi 22 baada ya mechi 11, sawa na vinara Barca, ambao waliduwazwa kwa bao 3 – 1 dhidi ya Levante mapema jana.

Atletico Madrid, ambao walicheza mechi moja ya ziada, wanakamata nafasi ya tatu, na pointi 21 baada ya kutoka sare ya 1 – 1 na Sevilla, ambao wako katika nafasi ya nne na pointi sawa na hizo.

Author: Bruce Amani