Real Madrid yaduwazwa nyumbani Bernabeu na Real Sociedad

Real Madrid wakiwa wachezaji 10 uwanjani wamepata kichapo cha kushangaza mikononi mwa Real Sociedad wakati wageni hao wakipata ushindi wao wa kwanza uwanjani Santiago Bernabeu katika La Liga baada ya miaka 15.

Willian Jose aliiweka Sociedad kifua mbele kupitia mkwaju wa penalty katika dakika ya tatu baada ya Mikel Merino kuangushwa na Casemiro wa Real Madrid.

Mambo kisha yakawa magumu kwa Real Madrid wakati Lucas Vazquez alipewa kadi nyekundu ikiwa imebaki nusu saa mchezo kuisha. Sociedad waliitumia vyema fursa hiyo wakati Ruben Pardo alitikisa wavu kwa njia ya kichwa na kuwapa ushindi wa 2-0.

Kichapo hicho kimeiacha Real Madrid katika nafasi ya tano wakati Sociedad ikisonga hadi nafasi ya 11.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends