Real Madrid yaichapa Granada 4-1 La Liga

Kikosi cha Real Madrid imerejea tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga baada ya ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Granada mchezo uliopigwa Jumapili Novemba 21.

Magoli ya Marco Asensio, Nacho yalitoa tumaini kwa kocha Carlo Ancelotti kabla ya Luis Suarez kufunga goli pekee kwenye mechi hiyo likiwa ni sawa na la kufutia machozi.

Magoli mengine ya ungwe ya pili kwa Madrid yakifungwa na Vinicius Junior ambaye alitumia vyema mpira wa kiungo fundi Luka Modric kabla ya Ferland Mendy kuhitimisha karamu ya magoli kwa Real Madrid.

Ushindi huo unaifanya Real Madrid kukwea mpaka nafasi ya kwanza wakiwa juu ya Real Sociedad na Sevilla wakati Granada wakishika nafasi za tatu kutoka chini.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends