Real Madrid yaongeza hofu kwa Atletico Madrid, yatoa kipigo cha 1-0 kwa Valladolid

Kikosi cha kocha Zinedine Zidane Real Madrid kimeongeza mbinyo kwa vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga baada ya kuondoka na alama tatu katika mchezo dhidi ya Real Valladolid katika ushindi wa goli 1-0 mchezo uliopigwa Jana Jumamosi.

Goli pekee kwenye mchezo huo limewekwa kimiani na kiungo mkabaji raia wa Brazil Casemiro akimalizia vyema mpira uliopigwa na kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Toni Kroos kunako dakika ya 65 na kubakiza alama tatu pekee kuwakamata vinara Atletico Madrid.

Hata hivyo, Madrid walionekana kuwa bora kwani kabla ya bao hilo fowadi Mariano Diaz aliweka mpira nyavuni mara mbili lakini yalikataliwa kuwa ni ya kuotea.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares