Real Madrid yapata ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Betis

52

Real Madrid imepata ushindi dhidi ya Real Betis na kusonga katika nafasi ya nne bora kwenye La Liga kwa kupata ushindi wa kwanza katika mechi tatu. Betis ilionekana kuponyoka na pointi moja kutokana na kazi yao kubwa hadi pale freekick ya Dani Ceballos ilipotua wavuni.

Real walipewa uongozi kupitia bao la Luka Modric, lakini timu mwenyeji iliudhibiti mchezo na kusawazisha kupitia Segio Canales baada ya uamuzi wa mchezaji kuotea kufutwa na mfumo wa VAR.

Madrid inapanda hadi nafasi ya nne, lakini wako nyuma ya vinara Barcelona na pengo la pointi 10.

Awali, Barca walipa ushindi wao wa saba mfululizo wa La Liga na kudumisha pengo la pointi tano kileleni mwa ligi dhidi ya nambari mbili Atletico Madrid waliopata ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Levante.

Real, mabingwa wa Ulaya katika misimu mitatu iliyopita, sasa wako nje ya kinyang’anyiro cha ubingwa wa ligi. wako nyuma ya nambari tatu Sevilla kwa tofauti ya mabao na pointi moja mbele ya Alaves katika nafasi ya tano.

Author: Bruce Amani