Real Madrid yapoteza, yaweka wazi mbio za ubingwa La Liga

Real Madrid imerudisha uhai wa mbio za ubingwa wa La Liga kuwa wazi kufuatia kuruhusu kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Real Betis ambapo sasa wanaiacha Barcelona kuwa vinara wa ligi kuu ya Hispania.

Barca ambao Jumamosi waliichapa Real Sociedad goli 1-0 walipanda mpaka nafasi ya kwanza alama mbili tofauti na kikosi cha kocha Zinedine Zidane.

Shuti la Sidnei liliipa uongozi Betis lakini dakika chache tena Karim Banzema akaweka mambo sawa kwa mkwaju wa penati, lakini dakika nane zikiwa zimesalia kuhitimisha mtanange huo strika za wazamani wa Barcelona Cristian Tello akafunga goli la ushindi kwa upande wa Betis.

Ushindi wa Betis ulikuwa na umuhimu kwao kwani umewatoa kutoka nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi mpaka nafasi ya 12.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments